- Mbunge huyo amesema kwa sasa hali yake ni nzuri
- Korir anasema alitibiwa na kushauriwa kwenda nyumbani
Mbunge wa Langata Nixon Korir amefunguka kuhusu jinsi anavyopambana na ugonjwa huo baada ya kuambukiwa wiki tatu zilizopita .Korir amefichua hali yake baada ya ripoti kuibuka kwamba amelazwa hospitalini akiugua virusi hivyo .
“ Nilipatikana na Corona wiki tatu zilziopita .lakini nimekuwa nikijitenga katika karantini nitakuwa nikipimwa tena kesho’ Korir ameliamvia gazeti la The Star .
Mbunge huyo chipukizi amesema pindi alipopatikana na virusi hivyo alikwenda hospitalini na kutibia kisha akarejea nyumbani kupata nafuu .
Amesema alipata daalili za ugonjwa huo katika siku za mwanzo mwanzo na akahudumiwa haraka na madaktari .
“ Nilipata baadhi ya daalili Novemba tarehe 1,2 na 3 kiwango hangu cha pumzi kilipungua lakini nikamudu kupata nafuu ,nilirejea nyumbani .
Amepuuza ripoti katika mitandao ya kijamii kwamna yungali hospitalini akiwa katika hali mahtuti .Amesema uvumi huo unaenezwa na wanablogi .