Muhtasari
- Amekuwa ICU kwa siku 10 tangu kuambukizwa ugonjwa huo
- Alikuwa mkuu wa kitengo cha maradhi ya figo KNH
Mkuu wa kitengo cha kutibu maradhi ya figo katika hospitali ya Kenyatta Dr Anthony Were Omolo amefariki kutokana na virusi vya corona
Dr Were aliaga dunia siku ya ijumaa usiku baada ya kuwa katika kitengo cha ICU kwa siku 10 ambapo amekuwa akipokea matibabu baada ya kuambukizwa ugonjwa huo .
Muungano wa madaktari umemtaja Were kama mwalimu na mtu aliyekuwa kielelezo kwa madaktari wengi . KMPDU imetuma risala za rambi rambi kwa familia yake .