Huduma za Treni

Wakaazi wa Athi River kupata huduma za treni kuanzia jumatatu

Wakaazi wa Athi River sasa wana chaguo la kutumia reli

Muhtasari

 

  •  Huduma hiyo imezinduliwa maajuzi na rais Uhuru 
  •   Huduma hizo za usafiri zitakuwa zikifanyika kila siku asubuhi na Jioni 

 

 

 Wakaazi wa  Athi River  kuanzia jumtatu watanufaika na huduma za usafiri wa treni zilizozinduliwa na rais Uhuru Kenyatta wiki jana

Abiria watalipa shilingi 80 kutoka Athi River hadi katika cha Reli  cha Nairobi . safari hiyo itachukua muda wa saa moja na dakika 23 kutoka kituo cha reli cha Athi River .

 Shirika la Reli siku ya ijumaa limetangaza kwamba  treni za usafiri wa abiria zitaanza oparesheni kwenda Athi River siku ya jumatatu  na ktoa ratiba ya safari hizo pamoja na gharama yake

 Kwa mujibu wa ratiba hiyo treni zitatoka  Athi River kila sik asubuhi saa  kumi na mbili alfajiri  na kusimama Mlolongo saa kumi na mbili na dakika 19 ,imara daima saa kumi na mbili na dakika 52  na makadara saa moja na dakika sita kabla ya kufika CBD saa moja na dakika 23 .

 Jioni treni itaondoka kituo cha Central saa kumi na moja na dakika 50  na kusimama  makadara saa kumi na mbili na akika tano ,Imara daina saa kumi na mbili na dakika 19 na kufika Athi River saa moja na dakika 13 jioni .

 Abiria  kutoka CBD  watalipa shilingi 50  iwapo watashukia makadara ,shilingi 50 wakishukia Imara Daima,shilingi 60 wakishukia mlolongo na shilingi 80 wakishukia Athi River