- Jumatatu Kinoti alikutana na waathiriwa wa ghasia za uchaguzi
- Amesema idara ya DCI itawachukulia hatua wote waliotekeleza ghasia na uhalifu wakati wa uchaguzi wa 2007/2008
Jumla ya kesi 72 za mauaji ,44 za kuhamishwa kutoka ardhi na vitisho 118 zinazohusiana na ghasia za baada ya uchaguzi tangu machafuko ya mwaka wa 2007/2008 amesema mkuu wa DCI George Kinoti
Kinoti ameahidi kwamba idara yake itafuatilia yote ambayo waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wwalimueleza baada ya kukutana nao siku ya jumatatu katika makao makuu ya DCI .
" Tunajua walionyakua mashamba yenu na mali yenu ambao sasa wametulia . Tunawajua walioua na ambao wanapita katika makaburi ya waliowaua ‘ amesema Kinoti .
Kinoti amesema serikali imeiagiza ofisi yake kuhakikisha kwamba hakuna ghasia au maafa yanatokea
" Hebu wajaribu tena . Tutafuata ukweli na kutayarisha faili za kuonyesha kwamba huyu ndiye aliyemuua mtu huyu’ amesema
" Hivi karibuni tutayaona matokeo ya hafla hii .Tutawatafuta .najua wanangoja uchaguzi mwingine ili kushuhudia ghasia’