Uuuzai wa watoto

Mkurugenzi wa matibabu wa NMS kushtakiwa kwa ulanguzi wa watoto

afisa mkuu wa Mama Lucy ameachiliwa huru

Muhtasari

 

  •  Sakata hiyo ilifichuliwa wiki jana katika makala ya BBC 
  •  Polisi wanasema waligundua kuwepo genge la kuiba na kuwauza watoto Nairobi 

 

 Mahakama moja ya Nairobi imeamuru kwamba naibu mkurugenzi wa huduma za matibabu katika NMS  Musa Mohammed na wafanyikazi wawili wa kijamii katika hospitali ya Mama Lucy washtakiwe kwa makosa ya ulanguzi wa watoto .

 Wafanyikazi hao wawili ni Makallah Fred na Selina Awuor .

 Hata hivyi mahakama imemuachiliwa huru afisa mkuu mtendaji wa hospitali hiyo Rmma Mutio .

 Wengi walioachiliwa huru na mahakama ni  Juliana Mbete, Beatrice Njambi  na  Regina Musembi.

 Upande wa mashtaka umesema umekamilisha uchunguzi na uko tayari kuwafungulia mashtaka watatu hao  . Musa hatajibu mashtaka dhidi yake kwa sababu mahakama imearifiwa kwamba anaugua na yupo katika hospitali kuu ya Kenyatta .

 Washukiwa hao sita walifikishwa mbele ya  hakimu mkuu Benard Ochoi siku ya jumatatu .washukiwa walifichuliwa baada ya kupeperushwa kwa Makala ya upekuzi ya BBC  yaliofichua sakata ya uuzaji wa watoto nchini .

 Washukiwa walikamatwa wiki jana baada ya polisi kuchunguza madai hayo na kugundua kuwepo genge ambalo lilikuwa likiwaiba na kuwauza watoto Nairobi .