Mkono wa Sheria

Mwenye nyumba ya Mountain View ambako watoto 44 wa shule walikamatwa katika karamu kuzuiliwa kwa siku 7

Watu wengine wawili pia wataalia seli kwa siku 7

Muhtasari
  •  wanafunzi 44 walikamatwa katika Nyumba ya Kithinji wakilewa siku ya jumamosi 
  •  Washukiwa wote watasalia rumande kwa siku saba ili polisi wakamilishe uchunguzi wao 

 

Mwenyeji wa karamuy ambako vijana 44 wadogo walikamatwa wakinywa pombe  katika mtaa wa mountain view na  watu wengine wawili watasalia rumande kwa siku saba ili uchunguzi ukamilishwe .

 Hii ni baada ya idara ya DCI kuitisha muda Zaidi ili kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo lililopeleka wanafunzi 44 na mmiliki wa nyumba hiyo Milicent Kithinji kukamaywa siku ya jumamosi .

 Wakati wa oparesheni hio  makachero walipata pombe na bangi katika nyumba hiyo . wanafunzi  hao wa shule za msingi na upili wakuwa 26 wavulana na wasichna 18  wote kati ya umri wa miaka 14 na 17

Kithinji,  mwenye umri wa miaka 41 alikamatwa na polisi ili kuhojiwa kuhusu karamu hiyo . uchunguzi wa mwanzo umeonyesha kwamba watoto hao walitoka sehemu mbali mbali ikiwemo  Machakos ,Kiambu na Narobi .

Kithinji  na washukiwa wengine wawili walifikishwa katika mahakama ya Milimani  wakati polisi walipotaka kupewa muda  wa siku saba Zaidi ili wakamilishwe uchunguzi wao

 Hata hivyo wakili wao  Kennedy cheruiyot alisema kwamba muda huo ni mrefu sana kwani Kithinji ana tatizo la kiafya .  Hakimu aliwaruhusu polisi kuwazuiliwa washukiwa wote kwa siaku saba .

 Jaji pia amewaagiza polisi kumrejesha Kithinji katika nyumba hiyo ili azichukue dawa zake