Watoto wanafanya mambo ya watu wazima

[PHOTOS] Tazama picha za nyumba ambamo watoto 44 walipatikana wakilewa

Haijafahamika mbona mshuikiwa mkuu aliwaruhusu watoto kulewa katika nyumba yake

Muhtasari
  •  Mshukiwa mkuu na watu wengine wawili wamefikishwa kortini leo 
  •  wakati wa oparesheni hiyo polisi walipata pombe ,bangi na mipira ya kondomu 

 

Watoto 44 wa shule  ya smingi na upili walikamatwa siku ya jumamosi katika nyumba moja mtaani Mountain View wakifanya karamu na kulewa ckari  .

 Pombe na dawa za kulevya ndio uraibu uliokuwa ukitawala hewa katika nyumba hiyo wakati polisi walipoivamia na kuvunja karamu

 Kulikuwa na  wavulana 26 na wasichana 18 walio na umri wa kati ya miaka 14 na 17 kutoka sehemu za Machakos ,Kiambu na Nairobi . Polisi wanashangaa jinsi watoto hao walivyosafiri kutoka sehemu mbali mbali bila wazazi wao kujua waliko wanao .

 Ishara kwamba watoto hao walikuwa na uhuru wa kushiriki kila uraibu wa utu uzima zipo wazi katika nyumbahiyo kwani kuna chupa zilizo bure za pombe ,na hata mipira ya kondomu ambayo imeshatumiwa ilipatikana .

 Mwenyeji wao ,mwanamke wa miaka 41 alikamatwa pia na maafisa wa kituo cha P[olisi cha Dagoretti na leo amefikishwa kortini pamoja na watu wengine wawili na watazuiliwa  rumande kwa siku saba zijazo