Waathiriwa wa machafuko ya zamani ya uchaguzi leo wataanza kurekodi taarifa zao katika makao makuu ya DCI .
Hii ni baada ya kuongezeka kwa hou ya ghasia kutoka kwa waathiriwa wa zamani wa machafuko ya baada ya uchaguzi . Uchunguzi wa mwanzo umebaini kuwepo vitisho na madhila dhidi ya waathiriwa hayo ambayo mkuu wa DCI George Kinoti atayazungumzia katika kikao na wanahabari saa nane alasiri siku ya jumatatu .
Watu 1,300 walifariki wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi kati ya wafuasi wa rais mstaafu Mwai Kibaki na kiongozi wa ODM Raila Odinga mwaka wa 2007
Wakili wa waathiriwa wa ghasia hizo katika mahakama ya ICC Fergal Gaynor, alisema watu aliopoteza mengi Zaidi katika mahaguko hayo nchii ni waathiriwa kwani kando na kupoteza maisha ya wapendwa wao,pia walipoteza mali yao .
Kufuatia ghasia za uchaguzi wa mwaka wa 2007/2008 naibu wa rais William Ruto alishtakiwa pamoja na mwanahabari Joshua Sang na aliyekuwa Mwenyekiti wa ODM Henry Kosgey
Mashtaka kama hayo pia yaliwakabili rais Uhuru Kenyatta ,aliyekuwa mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura na aliyekuwa kamishna wa polisi Hussein Ali .