DCI Mashakani?

DCI Matatani: Uhuru aonyesha ghadhabu kuhusu matamshi ya Kinoti na kesi za PEV

'Tumetoka huko na mambo haya tumezika katika kaburi ya sahau' -Uhuru

Muhtasari

 

  •  Firikia kwanza kabla ya kuzungumza ,rais amesema kuhusu hatua hiyo ya DCI 
  •  Kenyatta ameonekana kughadhabishwa na ripoti hizo kuhusu kufufuliwa kwa kesi za PEV 

 

Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta ameonekana kughadhabishwa na ripoti za hipi punde kwamba idara ya DCI inalenga kuzifufua kesi za ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007/2008 . Wakati wa uzinduzi wa ukusanyaji wa sahihi za BBI ,rais Kenyatta alionekana kukashifu hatua kama hizo akisema  ni   kujaribu kuhatarisha Amani ya nchi .

 Rais alisema ;

"Wale ambao wanajaribu kuchimbua makaburi, nilisoma kwa gazeti juzi, wasifikiri wanacheza. Mimi siwezi kukubaliana na mambo kama haya: tumetoka huko na mambo haya tumezika katika kaburi ya sahau. Kwa sababu ukijaribu kuleta maneno hapa, wewe hujui ni shida gani. Na wengine hawafikirii: You don't think before you talk, you don't think before you act. You must always think before you do something. Sisi hatutaki vita katika taifa letu la Kenya"

 Siku ya jumatatu mkuu wa DCI GeorgE Kinoti alikutana na watu kadhaa waliodaiwa kuwa waathiriwa wa ghasia hizo  hatua ambayo baadaye ilivutia hamaki ya wanasiasa wanaomuunga mkono naibu wa rais William Ruto waliodai kwamba Kinoti alikuwa na mpango wa kuzifufua kesi za ghasia za baada ya uchaguzi mwaka wa 2007/2008 .

 

Hatua hiyo ilizua hofu kwamba  itafungua tena uhasama kati ya jamii mbali mbali zinazoishi katika sehemu zilizokumbwa na ghasia hizo hasa Rift Valley . Rai Kenyatta katika hotuba yake amesema Kenya ingekuwa imeangamia iwapo yeye na kiongozi wa ODM Raila Odinga  hawangepatana kupitia mwafaka wa ‘Handshake’ . Naibu wa rais William Ruto akizungumzia   ripoti za Kinoti kukutana na waathiriwa wa gj]=hazia hizo alisema uamuzi  huo unlenga ‘kurejesha uhasama wa kikabila’ msimamo ambao rais leo ameonekana kuusisitiza .

 Kenyatta amesema marekebishi ya katiba ni mchakato ambao utakuwa ukiendelea  ili kuhakikisha kwamba sheria za nchi zinashughulikia matatizo ya wakati fulani