Mwafaka

Ruto asema bado kuna fursa ya kupata mwafaka kuhusu BBI

Ruto asema sio lazima pawepo ushindani kuhusu BBI

Muhtasari

 

  •  Ukusanyaji za sahihi za BBI umeanza leo 
  •  Ruto amesema sio lazima pawepo ushindani katika  kura ya maoni 

 

Naibu wa Rais William Ruto

 Naibu wa rais William Ruto ameshkilia kwamba bado kuna fursa ya mwafaka kupatikana kuhusu BBI  ili kuepuka kura ya maoni itakayozua ushindani  lichaya sahihi kuanza kukusanya siku ya jumatano kufanikisha marekebisho ya katiba .

 Kupitia twitter Ruto amesema  bado kuna uwezekano wa kuanda kura ya maoni ambayo sio lazima iwe na pande mbili za kunga mkono na kupinga .

 Katika ujumbe wake amesema kwamba umoja  ndio nguvu inayohitajika kukabiliana na mgogoro wa sasa wa janga la corona na kuboresha uchumi wan chi .

 Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga siku ya jumatano wamezindua ukusanyaji wa sahihi za BBI katika ukumbi wa KICC .

 Wakati wa hafla hiyo raia kenyatta alisisitiza kuhusu umuhimu wa handshake  akisema mwafaka huo ulizuia Kenya kutumbukia katika mgawanyiko zaidi .

Raila Odinga   anaye alaisema  masuala yanayohusu wananchi na hali ya uchumi yanaweza kushughulikiwa kupitia sheria na sera za serikali . Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa  ukusanyaji wa sahihi za BBI katika ukumbi wa KICC .

 Kuhusu wadhifa ya msimamizi wa idara ya mahakama ambalo limekuwa donda sugu katika ripoti ya BBI   Raila amesema  jopo la uteuzi litampa rais majina ya watu watatu ambao yatatumwa bungeni kupigwa msasa na kisha moja kuteuliwa na rais .

" Hilo litavuruga vipi  uhuru wa  idara ya mahakama? Raila amesema

" Tumepitia mengi ya uhasama na  siku ngumu  na hata vipindi vya kubaguliwa na tunaweza kuona tunakotaka kwenda’

 Amewahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi na kutia saini  zinazohitajika kufanikisha kura ya maoni ili kuirekebisha katiba .