Tanzia! aliyekuwa mbunge Mustafa Idd afariki

Muhtasari

• Ni mbunge wa zamani wa Kilifi Kusini.

• Alifariki akipokea matibabu katika hospitali ya Premier mjini Mombasa.

• Familia ilisema alikuwa na maradhi ya pumu.

Aliyekuwa mbunge wa Kilifi Kusini Mustafa Idd.
Aliyekuwa mbunge wa Kilifi Kusini Mustafa Idd.

Aliyekuwa mbunge wa Kilifi Kusini Mustafa Idd ameaga dunia.

Salid Idd  Mustafa ambaye alikuwa mwanahabari kabla ya kujitosa katika ulingo wa siasa alifariki akipokea matibabu katika hospitali ya Premier mjini Mombasa  mapema siku ya Jumatano.

Kufikia kifo chake alikuwa akihudumu kama mwenyekiti wa bodi ya ustawi wa maji katika kanda ya Pwani.

 

Binamuye Omar Kuta, alisema kwamba marehemu alipelekwa hospitalini kutokana na maradhi ya pumu.

“Mustafa amekuwa akiigua maradhi ya pumu lakini wakati huu hali yake ilikuwa mbaya zaidi na akakimbizwa hospitalini lakini kwa bahati mbaya alifariki mwendo wa saa tisa asubuhi,” Kuta alisema.

Mustafa mwenye umri wa miaka 50 alichaguliwa mbunge wa Kilfi Kusini kwa tiketi ya chama cha ODM mwaka 2013 baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2007. Hata hivyo alishindwa kutetea kiti hicho katika uchaguzi wa 2017 baada kukihama cha ODM na kujiunga na Jubilee.

Kabla ya kujiunga na siasa Mustafa alikuwa mtangazaji katika idhaa ya taifa KBC kabla ya kujiunga na NTV.

Atazikwa leo alasiri kuambatana na desturi za dini ya Kiislamu.