- Mudavadi amesifia mikakati iliyopendekezwa kulinda ugatuzi ,kutolewa kwa baraza la polisi na kulipa bunge la senate nguvu zaidi
- Kwa sababu ya hatua hiyo ANC Imeunda kundi lake la kuipigia debe ripoti ya BBI .
Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi sasa amesema anaunga mkono kikamilifu mapendekeo yaliyotolewa katika ripoti ya BBI na ataunga mkono kuandaliwa kwa kura ya maoni .
Mudavadi amesema chama chake kimepitia mapendekezo hayo ya BBI na kuamua kwamba ni mazuri kwani masuala yote walioibua yameshughulikiwa .
Mudavadi amesifia mikakati iliyopendekezwa kulinda ugatuzi ,kutolewa kwa baraza la polisi na kulipa bunge la senate nguvu zaidi
Kwa sababu ya hatua hiyo ANC Imeunda kundi lake la kuipigia debe ripoti ya BBI .
“ Tunataka kuzungumza na wakenya bila kutoa fursa ya watu kurushiana matusi .wakenya wanafaa kupewa fursa ya kujieleza.kwa hivyo tutazindua kundi letu kwanu hivi karibuni’ amesema Mudavadi
Akizungumza katika makao makuu ya ANC Mudavadi amesema kulindwa kwa Nairobi kama kaunti ni hatua itakayoboresha ugatuzi .
Amesema hatua hiyo itawapa wakaazi wa jiji fursa ya kuwachagua watu bora kushughulikia mahitaji yao .
Mudavadi amesema stakabadhi hiyo mpya inaonyesha kwamba mapendekezo yao yalitiliwa maanani .