Haki

Kesi ya mauaji ya wakili Willie Kimani yaahirishwa baada ya wakili Cliff Ombeta kuambukizwa Covid 19

Kesi hiyo imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara

Muhtasari

 

  •  Ombeta alifanyiwa vipimo siku ya jumapili na   matokeo yametolewa leo wakati kikao cha korti kilipotarajiwa kufanyika .
  •  Mwezi oktoba kesi hiyo iliahirishwa tena  baada ya mtuhumiwa mmoja Chebuert kupatikana na corona .
Wakili Cliff Ombeta

 Kesi ya mauaji ya wakili Willie Kimani imeahirishwa hadi jumanne baada ya mahakama kuambiwa kwamna wakili Cliff Ombeta ameambukizwa virusi vya Corona .

Ombeta anawaakilisha  Fredrick Leliman na Stephen Cheburet,  washtumiwa wawili katika esi hiyo ya mauaji .

 Jaji Jessie Lessit  ameelekeza  kwamba Ombeta aitumie korto matokeo siku ya jumanne . Korti iliarifiwa kwamba Ombeta alitangamana na mteja mmoja huko malindi  ambaye alipatikana na Corona na kulazwa hospitalini .

 Ombeta alifanyiwa vipimo siku ya jumapili na   matokeo yametolewa leo wakati kikao cha korti kilipotarajiwa kufanyika .

 Mwezi oktoba kesi hiyo iliahirishwa tena  baada ya mtuhumiwa mmoja Chebuert kupatikana na corona .

 Kesi hiyo ilifaa kusikizwa kupitia njia ya kidijitali  kutoka gereza la kamiti lakini Cheburet alisema alikuwa  akiugua .

Watuhumiwa wote walikuwepo isipokuwa Cheburet  ambaye aliitaka mahakama kuahirisha kikao hicho .Ombeta  aliwasiliana naye kupitia zoom  na kumuambia jaji  Lessit kwamba amepimwa mara tano na vipimo vyote vilionyesha kwamna ana  covid 19.