Somalia yatuma majeshi yake Mandera

Hofu yazuka baada ya Somalia kuyatuma majeshi yake katika mpaka wa Mandera

Mandera hutegemea sana Mogadishu kwa bidhaa za biashara ikizingatiwa kwamba ipo mbali na Nairobi .

Muhtasari

 

  •  Katika kaunti ya mandera wakaazi wameripoti kuwaona wanajseshi wa SNA wakichukua nafasi katika sehemu mbali mbali za mpaka wa pamoja kati ya Kenya na Somalia
  • Tangazo hilo lilijiri wakati rais uhuru kenyatta alipokuwa akifanya mazungumzo na mwenzake wa Somaliland  Muse Bihi  ambaye amefanya ziara rasmi Nairobi .

 

 Saa chache baada ya Somalia kutangaza kkatiza uhusiano wa kidiplomasia na Kenya ,nchi hiyi imewatuma manajeshi wake katika mpaka na Kenya katika eneo la Mandera .

 Katika kaunti ya mandera wakaazi wameripoti kuwaona wanajseshi wa SNA wakichukua nafasi katika sehemu mbali mbali za mpaka wa pamoja kati ya Kenya na Somalia .

 Hatua hiyo ya SNA imewapelekea baadhi ya wenyeji kuanza kuhama makwao wakihofia kuzuka kwa machafuko .afisa mmoja mkuu katika idara ya usalama huko Mandera  amethibitisha kuwasili kwa wanajshi wa Somalia mpakani .

 Waziri wa habari wa Somalia Osman Dubbe ametangaza mapema jumanne kwamba Somalia inakatiza uhusiano wa kidiplomasia na Kenya kwa sababu Kenya inaingia masuala yake ya ndani na kutishia  hadhi ya utaifa wake . Tangazo hilo lilijiri wakati rais uhuru kenyatta alipokuwa akifanya mazungumzo na mwenzake wa Somaliland  Muse Bihi  ambaye amefanya ziara rasmi Nairobi .

Mandera hutegemea sana Mogadishu kwa  bidhaa za biashara  ikizingatiwa kwamba ipo mbali na Nairobi .