Shule

Hakuna safari za Madaraka Express huku safari za kaunti moja hadi nyingine zikiongezwa shule zikifunguliwa jumatatu-Macharia

Amesema wanafunzi wamekuwa wakilishwa wakiwa nyumbani na wazazi hawafai kutarajia huduma kutolewa kwa wanao bila kuzilipia .

Muhtasari
  • Macharia  amesema  wizara yake imejadiliana na  sekta ya matatu ili kuhakikisha kwamba madreva wanapimwa kubaini Iwapo ni alevi kuzuia madreva walevi kuendesha magari  na wasipandishe nauli .
  • George Magoha amesema changamoto ya kutoweza kuwatenganisha wanafunzi madarasani haitazuia serikali kuendelea na mpango wake wa kufungua shule .
Waziri wa Uchukuzi Jmes Macharia

 Idadi  ya treni zinazosafiri kutoka kaunti moja hadi nyingine zitaongezwa kesho-mbili kutoka Nairobi na mbili kutoka  mmbasa kesho wakati wanafunzi wanapoanza kuripoti shuleni amesema waziri wa Uchukuzi James  Macharia .

  Hakutakuwa na safari za moja kwa moja za express  siku ya jumatatu  .treni hizo zitasimama katika vituo vyote 7 . waziri huyo aliyasema hayo siku ya jumapili katika kikao na wanahabari kilichowaleta pamoja mawaziri mbali mbali

Macharia  amesema  wizara yake imejadiliana na  sekta ya matatu ili kuhakikisha kwamba madreva wanapimwa kubaini Iwapo ni alevi kuzuia madreva walevi kuendesha magari  na wasipandishe nauli . wakati huo huo waziri wa elimu George Magoha amesema changamoto ya kutoweza kuwatenganisha wanafunzi madarasani haitazuia serikali kuendelea na mpango wake wa kufungua shule .

 Magoha amesema kila nafasi ya wazi shuleni itatumiwa kuwasomesha wanafunzi . Magoha amewaonya wazazi dhidi ya kukosa kulipa karo kwa msingi kwamba serikali ilikuwa imewaoya walimu kutowarejesha nyumbani wanafunzi wasio na karo . Amesema wanafunzi wamekuwa wakilishwa wakiwa nyumbani na wazazi hawafai kutarajia huduma kutolewa kwa wanao bila kuzilipia .