Vitisho

Polisi wachunguza vijakaratasi vya vitisho huko Kapsaret

Polisi wanachunguza waliosambaza vijikaratasi hivyo na kusema eneo hilo ni tulivu .Hakuna aliyekamatwa hadi kufikia sasa.

Muhtasari
  •  Kulingana na ripoti ya polisi  vijikaratasi hivyo vilitupwa katika kijiji cha  Mau Kipkaren .
  •  Vijikaratasi hivyo vikiwa na ujumbe ulioandikwa kwa Kiswahili vinawaonya wasio wenyeji  kutoka jamii nyingine kuondoka katika mashamba ya eneo hilo .
Vijikaratasi vya vitisho vilivyosambazwa Kipkaren

 Polisi katika  eneo  bunge la   Kapsaret  katika ya Uasin Gishu wanachunguza vijikaratasi vya vitisho vya kikabila ambavyo vimesambazwa  katika mtaa wa Kipkaren siku ya jumapili asubuhi .

 Kulingana na ripoti ya polisi  vijikaratasi hivyo vilitupwa katika kijiji cha  Mau Kipkaren .

 Vijikaratasi hivyo vikiwa na ujumbe ulioandikwa kwa Kiswahili vinawaonya wasio wenyeji  kutoka jamii nyingine kuondoka katika mashamba ya eneo hilo .

 Ujumbe huo umesema  "Kipkaren iko na wenyewe

"Na yale mashamba yameyaweka fence pia aguse aone moto. Hii ni 2021 hatutaki madoadoa Kipkaren

 Polisi wanachunguza waliosambaza vijikaratasi hivyo  na kusema eneo hilo ni tulivu .Hakuna aliyekamatwa hadi kufikia sasa.