Masomo chini ya Corona

( Katika Picha) Shule kote nchini zafunguliwa huku changamoto katikati ya janga la Corona zikianza kudhihirika

Wanafunzi kote walilazimika kuvalia maski

Muhtasari
  • Kesho jumanne wanafunzi Zaidi  wanatarajiwa kwenda shuleni kwani shule nyingi za kibinafasi zinafunguliwa  tarehe 5
  •   Maelfu ya wanafunzi waliraukia kuripoti shuleni huku walimu na wasimamisi wa shule wakiharakisha kufanya matayarisho ya jinsi masomo yatakavyoendelea chini ya hali hiyo ngumu inayolenga kuzuia maambukizi ya Corona .

 

Mwalimu akiwa darasani katika shule ya msingi ya Olympic ,Kibera katika siku ya kwanza ya shule kufunguliwa
Image: WILFRED NYANGARESI

 Shule zimefunguliwa siku ya jumatatu kote nchini huku wanafunzi katika baadhi ya shule  hizo wakilazimika kusomeshwa nje chini ya miti na mahema ili kuhakikisha kwamba hapana mirundiko madarasani katika siku ya kwanz aya kurejea shuleni tangu zilipofungwa mwezi machi kwa ajili ya Corona

  Maelfu ya wanafunzi waliraukia kuripoti shuleni huku walimu na wasimamisi wa shule wakiharakisha kufanya matayarisho ya jinsi masomo yatakavyoendelea chini ya hali hiyo ngumu inayolenga kuzuia maambukizi ya Corona .

Kesho jumanne wanafunzi zaidi  wanatarajiwa kwenda shuleni kwani shule nyingi za kibinafasi zinafunguliwa  tarehe 5 .Huu hapa msururu wa picha zinazoonyesha hali ilivyokuwa katika shule mbali mbali kote Kenya

 
Wanafunzi wa St.Monica wakiabiri matatu katika kituo cha mabasi cha Machakos ,shule zikifunguliwa tarehe nne Januari
Image: EZEKIEL AMING'A
Wanafunzi wa shule ya msingi ya New Kahumbuini wakiwasili shuleni mwao siku ya kufunguliwa . Takriban wanafunzi milioni 16 walirejea shuleni katika siku ya kwanza tangu shule kufungwa mwezi machi kwa ajili ya janga la corona
Image: ENOS TECHE
Wanafunzi wa shule ya wavulana ya Masimba wakiwa wamekwama katika kituo cha mabasi cha Machakos
Image: EZEKIEL AMING'A
Mwalimu akiwafunza wanafunzi hesabu katika siku ya kwanza ya kufunguliwa kwa shule
Image: DANIEL OGENDO
Wanafunzi wa grdi ya nne wa shule ya msingi ya Ogenya Nyando wakiwa katika sehemu waliotengewa kusoma baada ya shule yao kufurika maji
Image: DANIEL OGENDO
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Githunguri mtaani utawala Utawala wasajiliwa kabla ya kuingia shuleni
Image: Fredrick Omondi
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Githunguri Primary Utawala, Mavoko wakielekea shuleni
Image: Fredrick Omondi
Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Arya walazimika kusomea katika maktaba yapo baada ya madarasa kujaa
Abiria wakiwa wamekosa magari ya kusafiri kuwapeleka wanao shuleni .Nauli zimeongezeka mara dufu katika siku ya kwanza ya shule kufunguliwa
Image: DANIEL OGENDO
Wanafunzi wa St. Bhakita Primary wakiwasili shuleni katika siku ya kwanza ya shule kufunguliwa
Image: CHARLENE MALWA
Wanafunzi wa shule ya upili ya Ombaka wakisomea ndani ya mehama baada ya shule yao kuzama maji
Image: DANIEL OGENDO
Waziri wa Elimu George Magoha
Mwalimu akiwapima joto wanafunzi wakiripoti shuleni siku ya kwanza ya shule kufunguliwa