Jaji Mrima siku ya jumatatu amefutilia mbali arifa ya gazeti rasmi la serikali iliyotolewa na tume ya uchaguzi kutangaza uchaguzi mdogo wa ugavana Nairobi mwezi ujao .
Katika kesi hiyo gavana aliyetimuliwa madarakani Mike Sonko alikuwa amepinga kuondolewa kwake afisini akisema utaratibu ufaao haukufuatwa .
Maseneta waliidhinisha uamuzi wa waakilishi w kaunti kupiga kura ya kumuondoa Sonko afisini Disemba tarehe 17 .
Sonko alishtumiwa kwa kukiuka katiba ,kutumia vibaya maamlaka ya afisi yake na ukiukaji wa madili ya utendakazi