FBI yaonya wafuasi wa Trump huenda wakazua ghasia zaidi

Usalama umeimarishwa jkatika majengo ya bunge kufuatia ghasia zilizoshuhudiwa wiki iliyopita
Usalama umeimarishwa jkatika majengo ya bunge kufuatia ghasia zilizoshuhudiwa wiki iliyopita
Image: REUTERS

Shirika la upelelezi la Marekani FBI, limeonya kuhusu uwezekano wa maandaamnao yenye silaha kufanywa kote nchini siku chache kabla ya Joe Biden kuapishwa kuwa rais.

Kuna ripoti ya makundi yaliojihami yanapanga kukusanyika katika mabunge ya majimbo yote 50 na Washington DC kuelekea siku ya kuapishwa kwake Januari 20.

Hofu hiyo inajiri wakati mipango ya usalama imeimarishwa kwa ajili ya hafla hiyo.

 

Siku ya Jumatatu Bw. Biden aliwaambia wanahabari kwamba haogopi kula kiapo chao urais nje ya bunge la Marekani.

Yeye pamoja makamu wake mteule Kamala Harris bado wanatarajiwa kuapishwa nje ya jumba la Capital Hill, wiki mbili baada ya eneo hilo kuvamiwa na wafuasi sugu wa Rais Trump wanaopinga matokeo ya uchaguzi.

Maafisa wa usalama wamesisitiza hali iliyoshuhudiwa Januari 6 haitarudiwa tena- baada ya maelfu ya wafuasi wa Trump kufanikiwa kuingia katika majengo hayo wakati wabunge walikuwa wakipiga kura kuidhinisha matokeo ya uchaguzi.

Image: GETTY IMAGES

Chad Wolf, kaimu mkuu wa wizara ya usalama wa ndani, siku ya Jumatatu alisema ameagiza shirika la Upelelezi la Marekani kuanzisha oparesheni maalum ya maandalizi ya kumuapisha rais mpya Jumatano - siku sita kabla ya hafla yenyewe - "kutokana na tukio la wiki iliyopita linaloegemea masuala ya usalama. "

Maafisa wanasema hadi wanajeshi 15,000 wa kitaifa huenda wakatoa ulinzi wakati wa hafla hiyo.

 

Baadaye siku hiyo ya Jumatatu, Bw. Wolf alikuwa waziri wa tatu wa Trump kujiuzulu tangu kutokea kwa maandamano dhidi ya bunge, baada ya Betsy DeVos na Elaine Chao.

Kuondoka kwa Bw. Wolf kuliiweka wizara yake katika hali ya ngumu wakati inapojiandaa kusimamia usalama wakati Biden atakapoapishwa. Wiki iliyopita Bw. Wolf alitoa wito kwa Bw. Trump "kuwalaani vikali" waandamanaji waliovamia bunge.

Wazir huyo anayeondoka alisema hatua yake imechangiwa na "matukio ya hivi karibuni", ikiwa ni pamoja na maamuzi ya korti kupinga uhalali wa uteuzi wake kisheria.

Ni maandamano gani mengine yanapangwa?

Maafisa wa usalama wanasemekana kujiandaa kote nchini kuhusu uwezekano wa ghasia zaidi kutokea siku chahche kabla ya Joe Biden kuingia rasmi madarakani.

Ujumbe kutoka kwa mtandao wa wafuasi wa Trump na wale wa mrengo wa kulia umetoa wito wa maandamano katika miji kadhaa Januari 17 na matembezi kuelekea Washington DC siku ya kuapishwa rais mpya na makamu wake.

 

Taarifa ya ndani ya FBI, iliyoripotiwa na ABC News na vituo vingine vya habari imeonya kwamba kundi linalojiita ''kuvamia'' jimbo na majengo ya mahakama majimboni na kitaifa kote nchini ikiwa Bw. Trump ataondolewa madarakani mapema na siku ya kuapishwa ikiwa sio yeye atakaye apishwa.

Miito ya kumtaka Bw. Trump kujiuzulu, kuondolewa madarakani au kushtakiwa imeongezeka miongoni mwa Wademocrat na Warepublican siku kadhaa baada ya tukio la uvamizi wa bunge lakitaifa.

Mashirika ya polisi majimboni yameambiwa na maafisa wa ulinzi wa kuimarisha usalama katika ofisi za serikali kufuatia ghasia za wiki iliyopita, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Shirika la habari la Reuters, likimwashiria afisa wa ulinzi wa kitaifa, limesema onyo la FBI limetolewa kwa miji mikuu ya majimbo yote kuanzi Januari 16 hadi 20 mjini Washington DC kwenyewe angalau kwa siku tatu kablaya hafla ya kumuapisha rais mpya.

Japo taarifa ya uvamizi wa bunge la Marekani ziligonga vichwa vya habari wiki iliyopita, visa vingine vidogo sawia na hicho viliripotiwa katika maeneo mengine nchini wakati huo.

Ni usalmaa wa ain agani umewekwa siku ya kuapishwa kwa rais mpya?

Siku ya Jumatatu Wizara ya Usalama wa Ndani imethibitisha kwamba itaanza oparesheni maalum ya usalama wa kitaifa siku sita kabla hafla ya kuapishwa kwa rais mteule, kuanzi Jumatano.

Hatua hiyo itatoa nafasi kwa mashirika kadhaa ya usalama kushirikiana kutekeleza mipango kama ya kufunga bara bara na kuweka usalama kwenye maeneo yaliyozingirwa kuta za usalama.

Tangazo hilo limetolewa baada ya Meya wa Washington DC Bi Bowse, kutoa wito wa kuimarishwa kwa usalama baada ya kile alikiita "shambulio la ugaidi lisilokuwa la kawaida" katika bunge la Marekani wiki iliyopita.

Pia ametoa wito kwa kwa Wamarekani kujiepusha na usafiri wa kuja Washington DC kwa ajili ya hafla hiyo.

Sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya imekuwa ikiwavuti amamia ya watu katika barabara za mji mkuu, lakini janga la corona tayari lilikuwa limevuruga mipango hiyo kabla ya usalama kuimarishwa kutokana na hofu ya kutokea vurugu.