Joho yu wapi?Wahudumu wa afya wamtaka gavana kusitisha kimya chake

Muhtasari

• Mgomo wa wahudumu wa afya Mombasa umeingia siku ya 70

 • W hudumu wa afya wanamtaka gavana Joho kuingilia kati swala hili

 • Wahudumu wamesema hawatarejea kazini ikiwa matakwa yao hayatashuglikiwa

Gavana wa Mombasa Hassan Joho
Gavana wa Mombasa Hassan Joho

Huku mgomo wa wahudumu wa afya katika kaunti ya Mombasa ukiingia siku ya 70, wahudumu afya katika kaunti hiyo siku ya Jumanne walimtaka gavana Hassan Joho kusitisha kimya chake kuhusu swala hili.

Wakiongozwa na maafisa wa miungano mbali mbali ya waifanyikazi wa sekta ya afya, wahudumu hao walisema kwamba gavana wa Mombasa Hassan Joho amesalia kimya huku wao wakiendelea kuhangaishwa.

Mgomo wa wahudumu wa afya katika kaunti hiyo umelemaza utoaji wa huduma katika sekta hiyo huku wananchi wengi wanaotegemea hospitali za umma wakitaabika.

 
 

Peter Maroko kutoka muungano wa wauguzi alionya baraza la magavana dhidi ya kucheza siasa na Maisha ya wahudumu wa afya.

Alisema kamwe hawatarejea kazini ikiwa matakwa yao hayatashuglikiwa.

Alishangaa kwanini baraza  la magavana linaona ugumu kuzifidia famiilia za wenzao waliofariki kutokana na virusi vya COVID-19.

Alisema wahudumu wa afya ni kama tu watu wengine na kwamba hata wao wanahitaji kutunzwa na kukingwa dhidi ya maradhi na mambo mengine.

Naibu katibu mkuu wa muungano wa wauguzi nchini Maurice Opetu akihutubia wanahabari mjini Nairobi, alisema kwamba wauguzi na baadhi ya wahudumu wa Afya hawajapokea mshahara kutoka mwezi Novemba.

Viongozi hao walisema kwamba watashauri wanachama wake kupinga mchakato wa BBI ikiwa serikali haitalichukuliwa swala la makwa yao kwa uzito unaohitajika.