Covid-19:Mwanafunzi miongoni mwa watu 123 waliopatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 123 wapatikana na virusi vya corona huku 412 wakipona maradhi hayo
  • Mutahi alisema kwamba mwanafunzi ni miongoni mwa watu waliopatikana na virusi hivyo
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Watu 123 hii leo wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 98,555 hii ni baada ya sampuli 4,948 kupimwa chini ya saa 24.

Waziri wa wizara ya afya Mutahi Kagwe alisema kwamba mwanafunzi mmoja ni miongoni mwa watu ambao wamepatikana na corona kwa maana baba yake pia alipatikana na virusi hivyo.

Mutahi aliwauliza wazazi kuwaweka watoto wao nyumbani kama wanashuku wana virusi vya corona.

Kati ya maambukizi hayo mapya mgonjwa mwenye umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 85.

Watu 412 wamepona virusi hivyo huku idadi hiyo ikifika 81,667, 378 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku huku 34 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.