Jubilee kutowania kiti cha Machakos, Matungu na Kabuchai atangaza Tuju

Muhtasari
  • Jubilee kutowania kiti cha Machakos, Matungu na Kabuchai atangaza Tuju
  • Tuju alisema hii ni kutokana na umoja ambao umeletwa na maridhiano ya BBI

Katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju ametangaza kuwa chama hicho hakitakua na wawaniaji kiti katika uchaguzi mdogo wa Machakos,Matungu na Kabuchai.

Huku akizungumza siku ya Jumatano Tuju alidai kwaba uamuzi huo ni kutokana na umoja ambao umeletwa na ripoti ya maridhiano BBI.

Hata hivyo Tuju alisema kwamba chama hicho kitatoa mwaniaji wa kiti cha ugavana wa Nairobi endapo mahakama itakubali kuendelea kwa uchaguzi huo.

 

Tuju alisema nafasi za Jubilee zilijazwa na chama cha ANC na Ford Kenya ambazo ni rafiki za chama cha JUbilee.

"Tunafurahia ushiriki mzuri na Wiper,Ford enya na ANC ni uamuzi ambao umeleta picha kubwa ya kuleta nchi pamoja kupitia maridhiano ya BBI." Alisema Tuju.