Mwanafunzi wa kidato cha 2 akamatwa baada ya kujaribu kumkata naibu mwalimu mkuu na panga

Muhtasari
  • Mwanafunzi wa kidato cha 2 akamatwa baada ya kujaribu kumkata naibu mwalimu mkuu na panga
  • Mwalimu huyo aliokolewa na walimu wenzake na kumshika mwanafunzi huyo aliyekuwa ameficha panga kwenye mkoba wake wa shule

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya upili ya Mokwerero eneo la Kitutu Masaba ametiwa mbaroni baada ya kujaribu kumkata naibu mwalimu mkuu na panga.

Kulingana na Citizen Digital ripoti ya polisi ilionyesha kwamba mwalimu mkuu alimuita chifu wa mtaa huo na kumwambia kwamba mwanafunzi alikuwa anajaribu kufanya kitendo hicho.

Ripoti pia ilionysha kwamba mwanafunzi huyo wa miaka 18 alikuwa ameficha panga kwenye mkoba wake wa shule.

 

Mwalimu huyo aliokolewa na walimu wenzake baada ya kumshika mwanamfunzi huyo na kuarifu polisi.

Haya yanajiri saa chache baada ya mwanafunzi wa kidato cha 3 kuwadunga walimu wake na kisu kaunti ya Kisii.

Mwanafunzi huyo alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkaazi Mwandamizi Onchoro wakati aliposhtakiwa katika mahakama ya Kisii.

SRM Onchoro alimwachilia mshukiwa kwa dhamana ya Shilingi 100, 000 au dhamana ya pesa taslimu ya Shingi 50, 000 na mdhamini wa kiasi sawa au kupelekwa rumande ya watoto ya Manga Kaunti ya Nyamira kwasababu alikuwa mwanafunzi.