4 wafariki katika ajali ya ndege ya KDF

Muhtasari

  • Ilikuwa imetoka kambi ya wanahewa ya Eastleigh, mjini Nairobi kabla ya kuanguka katika mbugha ya Tsavo.

  • Idara ya jeshi, KDF kupitia akaunti yake ya Twitter siku ya Jumanne ilithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya asubuuhi.

Ndege ya KDF
Ndege ya KDF
Image: Maktaba

Watu wanne walihofiwa kufariki siku ya Jumanne jioni baada ya ndege ya jeshi aina ya helikopta iliyokuwa  na idadi ya watu isiyojulikana kuanguka katika eneo la Irima, kwenye mbuga ya Wanyama ya Tsavo Mashariki, kaunti ya Taita Taveta.

Idara ya jeshi, KDF kupitia akaunti yake ya Twitter siku ya Jumanne ilithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya asubuuhi.

Ndege hiyo ya idara ya jeshi la  wanamaji, muundo wa Harbin Y12 ilikuwa imetoka kambi ya wanahewa ya Eastleigh, mjini Nairobi kabla ya kuanguka katika mbugha.

"shughuli za uokoaji zinaendelea ," tweet ilisoma.

Afisa wa polisi wa ngazi ya juu katika eneo la Voi aliyetaka jina lake tulibane kwa sababu haruhusiwi kuzungumza na wanahabari alisema kwamba oparesheni ya uokoaji iliongozwa na maafisa wa huduma kwa wanyama pori na polisi wa kawaida.

Duru za jeshi ziliambia meza yetu ya habari kwamba ndege hiyo ilikuwa imetumwa kumchukuwa naibu mkuu wa majeshi Levi Mghalu aliyekuwa nyumbani kwake mjini Voi.