Vile shule zinawafilisi wazazi kwa ununuzi wa sare

Muhtasari

  • Baadhi ya shule zimewalazimisha wazazi kupata maski tano zenye nembo ya shule kwa shilingi 100 kila maski.

Wazazi na wanafunzi wanunua bidhaa kurudi shuleni
Wazazi na wanafunzi wanunua bidhaa kurudi shuleni

TAARIFA YA LEWIS NYAUNDI 

Shule zimekuwa zikiwalazimisha wazazi kununua sare kutoka kwa wauzaji wao waliyowachagua kwa bei za juu kuliko bei katika maduka ya kawaida.

Augizo hilo sio sahihi, inasema Mamlaka ya Ushindani nchini, Jumatatu ilionya shule dhidi ya kuwashurutisha wazazi pahali pa kununua sare na kuwashauri wazazi kuripoti kwenye tovuti yao shule ambazo zinashirikiana na wauzaji wa nguo na kulazimisha wazazi kununua sare kutoka kwao pekee.

Katika kisa cha hivi punde, meza yetu ya habari imebaini shule (jina limelibana) imewalazimisha wazazi kupata maski tano zenye nembo ya shule kama hitaji kwa wanafunzi wao kurudi darasani.

"Kila maski inagharimu Shilingi 100," mzazi mmoja aliiambia Star.

"kwa hivyo kila mzazi alilazimika kutoa shilingi 500 ili kukidhi mahitaji ya maski vitano."

Unyanyasaji wa wazazi kupitia shule kulazimisha wazazi kununua vifaa vya shule umekuwepo kwa muda kati ya wakuu wa shule na wauzaji fulani.

Wakati mwingine utapata kwamba wakuu wa shule wenyewe wanafanya biashara ya kusambaza sare na vifaa vingine vya shule.

Katika shule zingine, wanafunzi wamelazimika kununua sare mpya wanafunzi wanapoingia kidato cha 3, hata kama sare zao za zamani ziko katika hali nzuri.

 

Hakuna chaguo kwa wazazi / walezi / wanafunzi kununua sare kutoka kwa wauzaji wao wanaopendelea na wenye bei nafuu.

Masharti hayo yamekuwepo na bado yapo: shule hununua sare kutoka kwa wasambazaji wao waliochaguliwa kwa niaba ya wanafunzi na kurahisisha upatikanaji wa mmavazi.

Katika pita pita zetu tulibaini kwamba baadhi ya shule zinasisitza wanafunzi kununua sare wananunuzi waliyochaguliwa na shulje kwa shilingi 1,200 kwa longi badala ya shilingi 800 kwa maduka ya kawaida tuliyozuru mjini Nairobi.

Sketi za wanafunzi wa kike zinauzwa kkwa slingi 1,500 kwa kwa mahduka yanayopendelewa na shule badala ya shilingi 700 kwa maduka ya kawaida.

Mwenyekiti wa muungano wa wazazi nchini Nicholas  Maiyo alisema tatizo hilo limekuwepo kwa miaka mingi, na kuwataka wakuu wa shule kuacha kushirikiana na wauzaji kunyanyasa wazazi.

"Kawaida kiuchumi bidhaa zinaponunuliwa kwa wingi bei inapaswa kupunguzwa, lakini kwa bidhaa za shule mambo huwa tofauti wazazi hulazimishwa kwenda kwa maduka haya kununua bidhaa kwa bei za juu," Maiyo alisema.