Covid-19:Wagonjwa 683 hospitalini huku 166 wakipatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 166 wamepatikana na virusi vya corona huku idadi hiyo ikifika 98,859
  • Watu 3 wamepoteza maisha yao kutokana na corona
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Watu 166 hii leo wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 98,859hii ni baada ya sampuli 7,077 kupimwa chini ya saa 24.

Waziri wa wizara ya afya Mutahi Kagwe amesema kwamba 146 ni wakenya huku 20 wakiwa raia wa kigeni

Kati ya maambukizi hayo mapya100 ni wanaume huku 66 wakiwa ni wanake, mgonjwa mwenye umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 93.

 

Watu 262 wamepona virusi hivyo huku idadi hiyo ikifika 8,195,254 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku huku 8 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 3 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 1,726 watu walioga dunia kutokana na corona.

Vile vile wagonjwa 683 wamelazwa hospitali  tofauti nchini huku 1,712 wakippokea matibabu wakiwa nyumbani.

Wagonjwa 29 wamo katika wadi ya wagonjwa mahututi.