Covid-19: Hakuna maafa yoyote ya corona hii leo, 81 wakipatikana na virusi hivyo

Muhtasari
  • Watu 81 wapatikana na corona huku 51 wakipona maradhi hayo
  • Waziri wa afya Mutahi Kagwe amethibitisha kwamba leo hamna maafa yeyote kutokana na corona

Kenya hii leo imesajili visa 81 vipya vya maambukizi ya corona huku maambukizi ya maradhi hayo yakifikia 99,308.

Hii ni baada ya sampuli 2,347 kupimwa chini ya saa 24.

Kati ya maambukizi hayo mapya 68 ni wakenya huku 113wakiwa raia wa kigeni.

 

41 ni wanaume huku 40 wakiwa ni wanawake,mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 10 huku mwenye umri wa chini akiwa na miaka 98.

Vile vile watu 51 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 82,478 ya watu waliopona corona.

Watu 31 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 20 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Wagonjwa 694 wamelazwa hospitalini tofauti humu nchini huku 1,670 wakiwa wamejitenga nyumbani.

Pia wagonjwa 29 wamo katika wadi wa wagonjwa mahututi.