- Katibu wa Muungano wa wauguzi nchini tawi la Mombasa Peter Maroko amesema magavana hawafai kujilinganisha na wahudumu wa afya .
- " Tunachotaka ni marupurupu ya hali ngumu na hatari ya kazi yetu na sio nyongeza ya mishahara kama alivyodai mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya
Wahudumu wa afya Mombasa wanaitaka serikali ya kaunti kukoma kuingiza siasa na ubaguzi katika masuala yao na badala yake kushughulikia mamalamishi waliotoa ili kuboresha sekta ya afya .
Wahudumu hao wa afya wamekuwa wakigoma kwa wiki 11 na wamedai kwamba baraza la magavana limekuwa likitoa vitisho kwa wahudumu wa afya ,maafisa wa kliniki na wataalam wa maabara kurejea kazini bila kuongezwa malipo .
Katibu wa Muungano wa wauguzi nchini tawi la Mombasa Peter Maroko amesema magavana hawafai kujilinganisha na wahudumu wa afya .
" Tunachotaka ni marupurupu ya hali ngumu na hatari ya kazi yetu na sio nyongeza ya mishahara kama alivyodai mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya
Amesema kwamba sheria inahitaji wahudumu wa afya wafidiwe ifaavyo hasa kwa familia za waleambao waliaga dunia kwa ajili ya Corona wakiwa kazini . Ameongeza kwamba wafanyikazi wengi wa afya wameaga dunia tangu janga la corona kuripotiwa nchini ,hatua inayomaanisha kwamba kazi yao ni hatari .