Idara ya DCI imeanzisha rasmi mafunzo ya kozi mpya kuhusu uchunguzi wa uhalifu katika chuo chake .
Kozi hiyo maalum ya mafunzo kuhusu uchunguzi wa uhalifu inalenga kuwapa ujuzi maafisa hao kuweza kutumia njia za kitaalam kukabiliana na kesi za uhalifu zinazohitaji ujuzi wa hali ya juu .
Akiongoza uzinduzi wa kozi hiyo naibu mkurugenzi wa DCI Joseph shimala amesema kozi hiyo itakayowaleta pamoja maafisa 50 kutoka vitengo mbali mbali vya DCI itachukua muda wa wiki nane .
Kulingana na Ashimala maaafisa wa usalama wana jukumu kubwa la kukabiliana na changamoto zote wanazokabiliana nazo katika kutekeleza kazi yao .
Amesema ni jambo la kusikitisha kwamba baadhi ya wahalifu hukimbilia mahakama kupewa bondi za kibinafasi baada ya kufanya makosa kwani hatua hiyo inazuia kupatikana kwa haki .