Covid-19: Watu 136 wapatikana na corona huku idadi ya maambukizi hayo ikifika 99,444

Muhtasari
  • Watu 2 waaga dunia huku 136 wakipatikana na corona
  • Waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema kwamba watu 176 wamepona virusi hivyo
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Kenya hii leo imesajili visa 136 vipya vya maambukizi ya corona huku maambukizi ya maradhi hayo yakifikia 99,444.

Hii ni baada ya sampuli 3,787 kupimwa chini ya saa 24.

Kati ya maambukizi hayo mapya 117 ni wakenya huku 19 wakiwa raia wa kigeni.

85 ni wanaume huku 51 wakiwa ni wanawake,mgonjwa wa umri wa chini ana miaka miwili huku mwenye umri wa chini akiwa na miaka 98.

Vile vile watu 176 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 82,654 ya watu waliopona corona.

Watu 162 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 14 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Wagonjwa 686 wamelazwa hospitalini tofauti humu nchini huku 1,625 wakiwa wamejitenga nyumbani.

Pia wagonjwa 30 wamo katika wadi wa wagonjwa mahututi.

Pia hii leo watu wawili wamepoteza maisha yao huku idadi ya walioaga dunia ikifika 1,736.