Jaji Mkuu mpya

Idara ya mahakama yaanza kumsaka Jaji mkuu mpya

Mtu atakayefaulu kupewa kazi hiyo atakuwa na mshahara wa kati ya shilingi 990,000 na 1,327,888 bila kujumuisha marupurupu .

Muhtasari
  •  Mshikilizi wa nafasi hiyo ana jukumu la kuongoza iadara ya mahakama  ambayo ni kitengo cha tatu  cha serikali  na atahudumu pia kama mwenyekiti wa JSC na rais wa mahahakama ya juu zaidi
  •  Mwaka wa 2016   Maraga aliwapiku watu wengine 13 kumrithi Willy Mutunga  ambaye alistaafy mwaka mmoja mapema .
Makao makuu ya mahakama ya juu

 Idara ya mahakama imeanza kumtafuta jaji mkuu mpya ili kuiziba nafasi iliyoachwa wazi na  David Maraga . kupitia arifa ya gazeti asmi la serikali  iliyotiwa saini na kaimu jaji MKUU  Philomena Mwilu ,hatua hiyo inajiri wiki mja baada ya Maraga kustaafu .

 Notisi hiyo  inawaalika wanaotaka kuhudumu katika nafasi hiyo kutuma maombi ili kuzingatiwa  na tume ya huduma kwa idara  ya mahakama .

 Wanaotuma maombi wanafaa kuwa  mawakili wa mahakama kuu na uzoefu wa miaka 15  au kuwa jaji wa mahakama kuu au ya rufaa   au afisa wa idara ya mahakama na uzoefu na elimu inayotesheleza matakwa ya mshikilizi w anafasi hiyo .

 Miongoni mwa watu walioonyesha nia ya kutaka nafasi hiyo ni mkurugezi wa zamani wa mashtaka ya umma Philip Murgor . wengine ni naibu jaji mkuu Philomena Mwilu ,rais wa mahakama ya rufaa  William Ouko ,mwanasheria mkuu Kihara Kariuki na mtangulizi wake Githu Muigai .

 Mtu atakayefaulu kupewa kazi hiyo atakuwa na mshahara wa kati ya shilingi    990,000  na 1,327,888 bila kujumuisha  marupurupu . 

 Mshikilizi wa nafasi hiyo ana jukumu la kuongoza iadara ya mahakama  ambayo ni kitengo cha tatu  cha serikali  na atahudumu pia kama mwenyekiti wa JSC na rais wa mahahakama ya juu zaidi

 Mwaka wa 2016   Maraga aliwapiku watu wengine 13 kumrithi Willy Mutunga  ambaye alistaafy mwaka mmoja mapema .