- Katika video iliyowekwa youtube Trump alisema ‘ Nilipigavana vita vikali na kukabiliana na mengi kwa sababi hiyo ndio sababu mlionichagua’
- Bwana Trump hajakubali hadi sasa matokeo ya uchaguzi wa novemba iliyopita baada ya kushindwa na Joe Biden wa chama cha Democrat .
Rais anayeondoka wa Marekani Donald Trump ametoa hotuba yake ya kuiaga nchi baada ya miaka mine afisini akisema kwamba ‘Tumefanya tulichokja kufanya –na mengi zaidi’
Katika video iliyowekwa youtube Trump alisema ‘ Nilipigavana vita vikali na kukabiliana na mengi kwa sababi hiyo ndio sababu mlionichagua’
Bwana Trump hajakubali hadi sasa matokeo ya uchaguzi wa novemba iliyopita baada ya kushindwa na Joe Biden wa chama cha Democrat .
Bwana Biden ataapishwa jumatano ili kuchukua hatamu za uongozi . wiki mbili zilizopita zimekuwa ngumu kwa Trump baada ya tofauti kubwa kuibuka miongoni mwa wafuasi wake kutokana na uvamizi ulifanywa katika bunge la Congress na watu wanaomuunga mkono ili kuzuia wanachama wa bunge hilo kuidhinisha matokeo ya ushindi wa Biden .
" Ghasia za kisiasa ni shambulizi dhidi ya vyote tunavyoviamini kama wamarekani . Haziwezi kukubalika’ amesema Trump katika ujumbe huo wa video ambao hakumtaja mrithi wake kwa jina .
Bunge la Congress lilipiga kura kumfurusha afisini Trump kwa madai ya ‘kuunga mkono maasi’ na sasa senate itaanza vikao vya kujadili hoja hiyo na huenda akazuiwa kuwania wadhfa wowote wa umma . Ni rais wa kwanza wa Marekani kupigiwa kura ya kutokuwa na imani mara mbili . Trump aliratibu baadhi ya mafanikio yake akisema alifaulu kuujenga uchumi wa Marekani kuwa thabiti .
Anaondoka afisini huku kura za maoni zikionyesha kwamba ana uungwaji mkono wa asilimia 34 , kiwango cha chini sana kwa rais anayeacha maamlaka . Katika ujumbe huo wa dakika 20 Trump alisema utawala wake ulifanya kile ulichotaka kufanya na mengi zaidi.