Mkusanyiko wa matukio yote ya uhalifu jijini

Uhalifu: Mwanamume amdunga kisu mke wake na kisha kujiua Embakasi

Mwathiriwa alipiga kamsa na kusaidiwa na wahudumu wa boda boda waliowanasa washukiwa hao na kuwapa kichapo kabla ya polisi kuingilia kati na kuwaokoa

Muhtasari
  • Baadaye mshukiwa alijifungiua chumani mwao na kujidunga kisu kifuani na kuaga dunia papo hapo .
  •  Mtoto wa miezi miwili wa jamaa huyo na mke wake alikuwa kando yao na hakujerhiwa .Chanzo cha shambulizi hilo hakijajulikana .

Polisi wanachunguza tukio ambapo mwanamme mmoja katika eneo la Embakasi alimjeruhi mke wake kwa kumdunga kwa kisu na kisha kujiua . Jamaa huyo alitofautiana na mke katika mzozo wa kinyumbani na kutumia kisu cha jikoni kutekeleza shambulizi hilo  kwa kumdunga kisu mara saba kabla ya kujiua baadaye .

 Mwanamke huyo alikimbizwa katika hospitali ya Mama Lucy ambako anapokea matibabu .Polisi  wanasema jirani mmoja aliyejaribu kuingilia kati alijeruhiwa kwa kudungwa kisu na mshukiwa . Baadaye mshukiwa alijifungiua chumani mwao na kujidunga kisu kifuani na kuaga dunia papo hapo .

 Mtoto wa miezi miwili wa jamaa huyo na mke wake alikuwa kando yao na hakujerhiwa .Chanzo cha shambulizi hilo hakijajulikana .

 

 Huku hayo yakiarifiwa kundi la makachero  linachunguza iwapo wafanyikazi wa benki moja  jijini walihusika na tukio la wizi ambao washukiwa watatu wa ujambazi  walinusurika kuuawa na wananci muda mfupi baada ya kujaribu kutoroka na shilingi elfu 320 kutoka kwa mteja mmoja aliyekuwa ametoka kwenye benki hiyo siku ya jumanne .

 Mwanamme huyo alikuwa ametoka benki hiyo alipokutana na washukiwa hao watatu waliojitambulisha kama wafanyikazi wa kampuni moja ya simu wakati mmoja wao alipochukua mkoba uliokuwa na pesa hizo . Mwathiriwa alipiga kamsa na kusaidiwa na  wahudumu wa boda boda waliowanasa washukiwa hao na kuwapa kichapo kabla ya polisi kuingilia kati na kuwaokoa.