Covid-19: Maambukizi ya corona yafika 99,983 huku 4 wakipoteza maisha yao

Muhtasari
  • Watu 4 waaga dunia kutokana na corona huku 33 wakipona maradhi hayo

Kufikia jumapili ya leo idadi jumla ya maambukizi ya corona imefika 99,983baada ya watu 85 kupatikana na virusi hivyo.

Hii ni baada ya sampuli 2,985 kupimwa ndani ya saa 24 amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.

Kati ya maambukizi hayo mapya 69 ni wakenya huku 16 wakiwa raia wakigeni, pia kati ya maambukizi hayo 39 ni wanaume na 46 ni wanawake.

Pia kati ya maambukizi hayo Nairobi imerekodi visa 70 huku ikifuatiwa na kaunti ya Kiambu na visa 2.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 88.

Vile vile watu 33  wamepona maradhi ya corona huku idadi jumla ya waliopona ikifika 82,969, watu 25 wamepona wakiwa nyumbani huku 8 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Pia watu 4 wamepoteza maisha yao kutokana na corona huku idadi hiyo ikifika 1,744.

Huku hayo yakijiri wagonjwa 545 wamelazwa hospitalini mbali mbali huku 1,568 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.