- Madai hayo yalisababisha mgogoro wa kidiplomasia kati ya Kenya na Somalia na kila nchi ikawaita nyumbani mabalozi wake .
- Somalia imekuwa ikishikilia kwamba Kenya inaingilia masuala yake ya ndani kuifanya dhaifu
Kundi lililoteuliwa kuchunguza madai ya omalia kwamba Kenya inaingilia masuala yake ya ndani na kuyahami makundi ya wapiganaji limesema hakuna usahidi kwamba Kenya inahusika na vitendo kama hivyo .
Madai hayo yalisababisha mgogoro wa kidiplomasia kati ya Kenya na Somalia na kila nchi ikawaita nyumbani mabalozi wake .
“ Tume imepata kwamba madai haya mengine yakiwa lalama za muda mrefu hayana ushahidi wa kusababisha mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili . Ni kweli kwamba Somlia ni nchi huru na maamuzi yake yanachukuliwa kwa msingi huo’ sehemu moja ya ripoti hiyo imesema
" Hata hivyo kwa uangalizi wa karibu madai hayo hayasaidii kwani nchi hizi mbili zina uhusiano wa karibu kisiasa ,kiuchumi na kiutu’
Ripoti hiyo imeongeza kwamba kutokana na mzozo huo wa kidiplomasia watoto 3000 wa Somalia wanaosomea Kenya hawakuweza kwenda shuleni na pia mzozo huo ulivuruga oparesheni za wanajeshi wa Amisom ,kuvuruga biashara ya miraa na oparesheni za kutoa misaada .