Corona

2 wafariki huku 99 wakipatikana Corona

Kutoka visa hivyo 99 vilivyoripotiwa 80 ni wakenya ilhali 19 ni raia wa kigeni .

Muhtasari
  •  Leo watu 66 wamepona ugonjwa  huo na kufikisha 83,757 idadi ya waliopona Corona .
  • Watu wawili wameaga dunia na kufikisha 1,753  idadi ya waliofariki kwa ajili ya ugonjwa huo.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

 Watu 99 wamepatikana na virusi vya Corona  baada ya sampuli 4,758  kupimwa katika saa 24 zilizopita. Jumla ya visa vya ugonjwa huo sasa  vimefika 100,422.idadi ya sampuli zilizopimwa sasa ni 1,172,167  .

Kutoka  visa hivyo 99 vilivyoripotiwa 80 ni wakenya ilhali 19 ni raia wa kigeni .62 ni  wanaume ilhali 37 ni wanawake mgonjwa wa umri wa chini ana miaka mitano ilhali aliye na umri wa juu ana miaka 88 .

 Leo watu 66 wamepona ugonjwa  huo na kufikisha 83,757 idadi ya waliopona Corona .

Watu wawili wameaga dunia na kufikisha 1,753  idadi ya waliofariki kwa ajili ya ugonjwa huo.

 Kuna wagonjwa  476 ambao  wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini ilhali 1,363 wapo  chini ya mpango wa utunzi wa nyumbani .Wagonjwa 28 wapo ICU  ilhali 5 wapo katika kitengo cha HDU