Moto

Bunge la Garissa lateketea katika mkasa wa moto wa asubuhi

Karani wa bunge hilo Mohamed Santur ametaja hasara iliyosababisha na mkasa huo wa moto kama ‘Kubwa’

Muhtasari
  •  “ Nilipofika nilimpata mlinzi mmoja akijaribu kuuzima moto huo .Nilimsaidia lakini tulizidiwa na kiasi cha moto uliokuwa ukiwaka’ amesema Abdi .
  • Joseph Wambua,  mhudumu wa boda boda alijutia kwamba wazima moto wlaichukua muda mrefu-takriban dakika 45 kujibu tukio hilo na kufanya moto huo kusambaa kwa afisi zilizo karibu
Bunge la kaunti ya Garissa likichomeka
Image: Stephen Astarika

Bunge la kaunti ya Garissa na afisi zilizo karibu zimeteketea mapema leo katika kisa cha moto ambao chanzo chake hakijajulikana .

 Tukio hilo mwendo wa saa mbili na dakika 20  kilitokea wakati mto ulipozuka katika  bunge la kaunti na kusambaa hadi katika afisi zilzio karibu . Ilichukua dakika 45 kwa zima moto wa Garissa kufika eneo la mkasa licha ya kuwa umbali wa kilomita 5 kutoka majengo ya bunge hilo .

 Juhudi za wananchi  kujaribu kuuzima moto huo ziliambulia patupu kwa sababu sakafu ya jengo hilo imewambwa kwa  vitambaa vya  nguo na  dari ni la mbao zilizopigwa rangi .

 Waokoaji  pia walifaulu kuliondoa gari ambao lilikuwa kkaribu na jengo hilo  ili kulipeusha na hasara ya kuchomeka . Mohamed Abdi  mlinzi katika duka zilizo karibu amesema aliona moshi mweusi ukitokea katika jengo la bunge na kisha akakimbia kutazama kilichokuwa kikifanyika .

 “ Nilipofika nilimpata mlinzi mmoja akijaribu kuuzima moto huo .Nilimsaidia lakini tulizidiwa na kiasi cha moto uliokuwa ukiwaka’ amesema Abdi .

Joseph Wambua,  mhudumu wa boda boda alijutia kwamba wazima moto wlaichukua muda mrefu-takriban dakika 45 kujibu tukio hilo na kufanya moto huo kusambaa kwa afisi zilizo karibu

 Karani wa bunge hilo Mohamed Santur ametaja hasara iliyosababisha na mkasa huo wa moto kama ‘Kubwa’