Kifo cha Kabaka

Korti yatupilia mbali kesi dhidi ya mwalimu aliyehusishwa na kifo cha seneta Kabaka

Mahakama siku ya alhamisi ilifutilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Bi Esther Muli .

Muhtasari
  • Hii ni baada ya DPP  kuwasilisha ombi la kuiondoa kesi hiyo akisema ushahidi ulitolewa haukumuweka mtuhumiwa katika eneo la kifo cha marehemu Kabaka .
  •  Hakimu mkuu David Ndungi akimuachilia  Muli amesema amezingatia ombi lililotolewa na  Mkurugenzi wa mashtaka ya umma .

 

Esther Nthenya

 Mahakama ya Nairobi imetupilia mbali kesi dhidi ya mwalimu aliyehusishwa na kifo cha seneta wa  machakos  Boniface Kabaka ambaye alikuwa amezuiliwa na kisha kuachiliwa huru baadaye  kwa sababu ya ukosefu wa ushahidi .

 Mahakama siku ya alhamisi  ilifutilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili  Bi Esther Muli . Hii ni baada ya DPP  kuwasilisha ombi la kuiondoa kesi hiyo akisema ushahidi ulitolewa haukumuweka mtuhumiwa katika eneo la kifo cha marehemu Kabaka .

 Upande wa mashtaka umesema uchunguzi wa watalaam umebaini kwamba  hakuna ushahidi unaomhusisha mshukiwa na kifo cha kabaka 

 Hakimu mkuu David Ndungi akimuachilia  Muli amesema amezingatia ombi lililotolewa na  Mkurugenzi wa mashtaka ya umma .