- Mageuzi hayo yametangazwa kupitia arifa ya ndani iliyotolewa januari tarehe 27 ikiorodhesha wale walioathiriwa
- Polisi wa trafiki ndio hulaumiwa sana kwa maovu katika huduma ya polisi kwa sababu ya kazi yao
Zaidi ya maafisa 120 wa polisi wa trafiki wamehamaishwa katika mageuzi yanayolenga kuboresha oparesheni za idara hiyo kote nchini .
Maafisa waliohamishwa ni kutoka Baringo, Uasin Gishu, Narok, West Pokot, Kericho, Nandi, Nakuru, Kajiado, Trans Nzoia, Laikipia na Bomet
Polisi hao walihamishwa kutekeleza majukumu ya kawaida baada yaw engine kukumbwa na visa vya ukosefu waidhamu na ukiukaji wa madili ya utendakazi katika idra ya trafiki . Mageuzi hayo yametangazwa kupitia arifa ya ndani iliyotolewa januari tarehe 27 ikiorodhesha wale walioathiriwa
Polisi wa trafiki ndio hulaumiwa sana kwa maovu katika huduma ya polisi kwa sababu ya kazi yao . wakati mwingine wao hujipata katika hali ngumu kwa kushambuliwa na wenye magari wakishtumiwa kwa kuwa wakali ama kuwaonea wenye magari kwa kuitish kiasi kikubwa cha faini kwa makosa madogo madogo .
Siku ya jumanne rais Uhuru Kenyatta alisema polisi sio adui wa raia na kuwahimiza wananchi kushirikiana nao ili kuhakikisha kwamba wakenya wote wako salama .
Mageuzi hayo yamejiri siku chache tu baada ya makao makuu ya idara hiyo kuanya polisi dhidi ya kuweka vizuizi kwenye barabara kuu nchini . vizuizi hivyo aghalabu vinatumiwa kama vituo vya kuwapunja fedha wenye magari na hivyo inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai anataka vizuizi vya muda tu .