Polisi wamejiunga na jeshi kuchunguza tukio ambapo afisa mmoa wa KDF amejiua katika nyumba yake Lanet ,Nakuru .
Afisa huyo wa cheo cha Major anahudumu katika 81 Tank Battalion kwenye kambi ya jeshi ya Lanet na alipatikana katika choo cheke baada ya kujikata shingoni .
Alitumia kisu cha jikoni kujiua . Alikuwa amevalia sare rasi ya kazi na alipatikana amelowa damu yake baada ya tukio hilo kufanyika siku ya jumatno usiku
Polisi wa jeshi waliwaarifu polisi wa kawaida kuhusu tukio hilo . Kilichosababisha afisa huyo wa KDF kujiua hakijajulikana na mwili wake umepelekwa katika hifadhi ya mati katika eneo hilo kufanyiwa uchunguzi .
Visa vya maafisa wanaohudumu katika idara za usalama na ulinzi vimezidi . maafisa wake katika idara hizo hukumbwa na msonono kwa sababu ya kazi yao .kwa wanajeshi ,kuna vituo maalum katika kami zao ili kuwapa usaidizi wa kisaikolojia .