Ukatili

Polisi wamsaka Mwanamume aliyembaka na kumpachika mimba msichana wa miaka 13 Makueni

" Iwapo kuna aliye na Habari kuhusu aliko tafadhali piga simu kwa nambari 0800 722 203 kwa hatua kuchukuliwa ," amesema mkuu wa DCI George Kinoti

Muhtasari
  •  Akiwa shuleni msichana huyo mwenye umri wa miaka 13 katika shule ya  Kathonzweni Holy Ghost  alikuwa amelalamikia maumivu ya tumbo
  •  Mwezi jana  kisa kama hicho kiliripotiwa huko Meru ambapo mhudumu wa boda boda alidaiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 8

Msako umeanzishwa dhidi ya mwanammme mwenye umri wa miaka 31 aliyemdhuylumu kimapenzi na kumpachika mimba msichana mwenye umri wa miaka 13 wa shule huko Makueni.

 Akiwa shuleni msichana huyo mwenye umri wa miaka 13 katika shule ya  Kathonzweni Holy Ghost  alikuwa amelalamikia maumivu ya tumbo . Shule ilimuita mamake kumpleka hospitalini  na baada ya kukaguliwa iligunduliwa kuwa alikuwa na uja uzito  baada ya kufichua kwamba alidhulumiwa kimapenzi na mshukiwa .

 Mshukiwa aliyetambuliwa kama Reuben  Mutie kwa lokesheni wa Kwa kavisi alitambuliwa kama aliyetekeleza kitendo hicho na akakwepa

" Iwapo kuna aliye na Habari kuhusu aliko tafadhali piga simu kwa nambari  0800 722 203  kwa hatua kuchukuliwa ," amesema mkuu wa DCI George  Kinoti

 Mwezi jana  kisa kama hicho kiliripotiwa huko Meru ambapo mhudumu wa boda boda alidaiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 8

  Polisi wanasema mshukiwa alijitolea kumsafirisha mtoto huyo kwenda kwao  katika eneo la Baibariu Igembe kusini lakini njia akabadilisha mipango na kumpeleka kwake ambako alitekeleza kitendo hicho . Baadaye alimpeleka mtoto huyo karibu na nyumbani kwao kabla ya kukwepa na kujificha  .Kisa hicho kilitokea siku moja baada ya afisa wa KDF Kukamatwa kwa kumbaka mtoto .