Tanga tanga nje

Washirika wa Ruto kutoka Mlima Kenya wafungiwa nje ya mkutano wa rais Uhuru Sagana

“ Sijapokea mwaliko hadi sasa . watu watakaosafirishwa kutoka maeneo mbali mbali ya Kati hawatamuambia rais ukweli’.

Muhtasari
  •  Kufikia siku ya jumatano  viongozi hao walikuwa wameshawatambua waakilishi wa kibiashara ,vijana ,miungano ya walimu na viongozi wa kidini ambao watahudhuria mkutano huo sagana .
  •  Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ameliambia gazeti la The star kupitia simu kwamba   mkutano huo hautaafikia lolote  kwani  ‘rais atakuwa akiwahubiria watu ambao tayari wamebadilishwa’
Naibu wa rais William Ruto na wabunge wanaomuunga mkono

Washirika wa naibu wa rais William Ruto kutoka mlima Kenya wameachwa nje ya mkutano wa rais Uhuru Kenyatta huko Sagana   utakaofanywa siku ya jumamosi , mkutano huo wa mashauriano wa viongozi kutoka mlima Kenya  unalenga kuhakikisha kwamba viongozi hao wanashirikiana kutangaza ripoti ya BBI na kuwashaiwshi wenyeji kukubali ripoti hiyo .

 Katika ishara nyingine kwamba rais hayuko tayari kufanya kazi na washirika wa Ruto ,utawala wa mikoa na viongozi wa mrengo wa kieleweke wametakiwa kuwatambua watu wa kuhudhuria mkutano huo .

 Kufikia siku ya jumatano  viongozi hao walikuwa wameshawatambua waakilishi wa kibiashara ,vijana ,miungano ya walimu na viongozi wa kidini ambao watahudhuria mkutano huo sagana .

 Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ameliambia gazeti la The star kupitia simu kwamba   mkutano huo hautaafikia lolote  kwani  ‘rais atakuwa akiwahubiria watu ambao tayari wamebadilishwa’

 Mbunge huyo ambaye ni mshirika wa karibu wa Ruto  amesema BBI haina umaarufu miongoni mwa wakaazi wa mlima Kenya .

“ Sijapokea mwaliko hadi sasa . watu watakaosafirishwa kutoka maeneo mbali mbali ya Kati hawatamuambia rais ukweli’.

 Seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata  alizua joto la kisiasa katika eneo la Kati kwa kumuandikia barua rais akieleza kwamba huenda ripoti ya BBI itaangushwa na wakaazi wa eneo la mlima kenya .