Uongozi wa idara ya mahakama

Uamuzi dhidi ya Mwilu ni ‘ugaidi wa idara ya mahakama,ukandamizaji-Orengo

Orengo amedai kuna njama ya kumzuia Mwilu kumrithi mtangulizi wake David Maraga

Muhtasari
  •  Seneta  Orengo hata hivyo  amesema uamuzi hu unamaanisha kwamba mfumo wa sheria umevunjika  na  utovu wa madili umeingia katika idara ya mahakama .
  •  Rais wa chama cha wanasheria LSK Nelson Havi ametaka kuondolewa kwa jaji Patrick Otieno aliyetoa uamuzi huo kwa ukiukaji wa madili .

 

Seneta wa Siaya James Orengo

  Agizo la mahakama linalomzuia naibu jaji mkuu kutohudumu kama   jaji mkuu  ni kitendo cha ugaidi wa idara ya mahakama  amesema seneta wa Siaya  James  Orengo .

 Mahakama kuu  ya Meru siku ya ijumaa ilitoa maagizo  ambayo ynamzuia Mwilu kuhudumu kama kaimu jaji mkuu na mwenyekiti wa  tume ya JSC    katika kesi inayotilia shaka hadhi yake .

 Mlalamishi alidai kwamba Mwilu anakabiliwa na kesi  ya ufisadi na itakuwa mapendeleo kumruhusu kuendelea kuhudumu kama mwanachama na rais wa  mahakama ya juu Zaidi

 Seneta  Orengo hata hivyo  amesema uamuzi hu unamaanisha kwamba mfumo wa sheria umevunjika  na  utovu wa madili umeingia katika idara ya mahakama .

 Ukosoaji wa orengo kuhusu uamuzi huo  sasa unashehei msururu wa maoni kama hayo na pingamizi kutoka kwa  baadhi ya watu   umetajwa kama njama ya baadhi ya watu kupunguza  nguvu ya idara ya mahakama .

 Rais wa chama cha wanasheria LSK Nelson Havi ametaka kuondolewa kwa jaji Patrick Otieno aliyetoa uamuzi huo kwa ukiukaji wa madili .