Mkusanyiko wa habari za uhalifu

Mwanamme amuua mkewe na watoto wao wawili Mbeere

.Baadaye mshukiwa huyo alijaribu kujiua kwa kuruka kutoka jengo la ghrofa tano mtaani Kayole

Muhtasari
  •  Tukio hilo lilifanyika jumapili asubuhi   wakati mshukiwa alipojifungia chumbani na kutekeleza mauaji hayo  .
  • Chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana

 Polisi huko Mbeere  wanachunguza kisa ambapo mwanmme mmoja amewaua mkewe na wanawe wawili  .Idara ya DCI imesema  mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 aliuawa na mume wake  pamoja na watoto wawili wenye umri  wa miaka  tisa na nane .

 Tukio hilo lilifanyika jumapili asubuhi   wakati mshukiwa alipojifungia chumbani na kutekeleza mauaji hayo  .Chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana

 Huku hayo yakiarifiwa polisi mtaani Kayole  wamepiga hatua  mwishoni mwa wiki katika kupata ushahidi kuhusu mauaji ya mwanamme mmoja Margaret Muchemi.Mwanamke huyo  aliteketezwa ndani ya nyumba yake na mpenzi wake kabla ya wili wake kupatikana baadaye .

 Mwishoni mwa wiki polisi wanasema walipata  simu ya mshukiwa iliyokuwa imefichwa katika duka moja la kuuza vileo katika mtaa wa umoja  linalomikiliwa na mshukiwa anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo Charles Oluenyi.

Alikamatwa januari tarehe 27  kuhusiana na mauaji hayo  baada ya kutoroka kwa Zaidi ya wiki moja  tangu mauaji hayo kuripotiwa januari tarehe 21 .Baadaye mshukiwa huyo alijaribu kujiua kwa kuruka kutoka jengo la ghrofa tano mtaani Kayole