Muhtasari
- Mkuu wa DCI George Kinoti amesema Kipkogei alipatikana katika maficho yake Ray Farm Uasin Gishu siku ya jumamosi alasiri
- Kipkogei na ndugu yake mwingine ambaye hajakamatwa walimshambulia kaka yao mdogo na kumuua kwa sababu ya utata kuhusu umiliki wa shamba
Mwanamme ambaye amekuwa mafichoni kwa kushukiwa kumuua kakake kwa sababu ya mzozo kuhusu umiliki wa shamba amekamatwa .
Alex Kipkogei, 37, anashtumiwa kwa kumuua kakake mdogo baada ya mzozo huko huko Chesitek-Keiyo North.
Mkuu wa DCI George Kinoti amesema Kipkogei alipatikana katika maficho yake Ray Farm Uasin Gishu siku ya jumamosi alasiri
Kipkogei na ndugu yake mwingine ambaye hajakamatwa walimshambulia kaka yao mdogo na kumuua kwa sababu ya utata kuhusu umiliki wa shamba . Mshukiwa atafikishwa kortini siku ya jumatatu huku polisi wakiendelea kumsaka mshukiwa wa pili aliyetajwa kama John Lotema.
" Iwapo una Habari zitakazopelekea kukamatwa kwake tafadhali piga simu kwa nambari isiokuwa na tozo 0800 722 203," Kinoti amesema