Nyachae kuzikwa leo

Usalama waimarishwa kabla mazishi ya Simeon Nyachae leo

Alimtaja Nyachae kama kiongozi aliyependa Amani .

Muhtasari
  •  Matiang’I amesema Nyache atapewa taadhima ya kupewa maziko ya kitaifa . Viongozi wakuu serikalini  watahudhuria hafla ya mazishi ya Nyache katika uwaja wa Gusii .
  •  Mwili wa Simeon Nyachae uliwasili jana katika boma lake ,Nyosia Kisii .
Mwili wa Nyache wawasili katika boma lakela Nyosia
Image: ANGWENYI GICHANA

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi amesema usalama utaimarishwa wakati  wa mazishi ya waziri wa zamani Simeon  Nyachae  anayezikwa leo jumatatu huko Kisii

Matiang'i  amesema rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ni miongoni mwa watakaohudhuria mazishi hayo .Aliyasema hayo siku ya jumapili  alipzuru uwanja wa Gusii .

  Matiang’I alikuwa ameandamana na gavana wa Kisii  James Ongwa ,mwakilishi wa akina mama Janet Ongera ,katibu wa kudumu wa afya Susan Mochache na viongozi wengine kutoka eneo hilo kabla ya mazishi hayo baadaye leo .

 Matiang’I amesema Nyache atapewa taadhima ya kupewa maziko ya kitaifa . Viongozi wakuu serikalini  watahudhuria hafla ya mazishi ya Nyache katika uwaja wa Gusii .

" Tunataraji kumpa maziko ya utulivu na amai kiongozi  huyo wetu .Kila kitu kiko tayari ,mahema yamewekwa ‘ Matiang’I aliwaambia wanahabari .

 Alimtaja Nyachae kama kiongozi aliyependa Amani .

 Sehemu ambako misa ya mazishi itafanyika imebadilishwa kutoka  uwanja wa michezo wa  Nyanturago  hadi uwanja wa Gusii  kwa sababu ya idadi kubwa ya wanaotarajiwa kuhudhuria .

 Mwili wa Simeon Nyachae uliwasili jana katika boma lake ,Nyosia Kisii .