Philomena Mwilu ameteua Benchi la majaji watatu kusikiliza maombi yaliyowasilishwa dhidi ya DG Kananu

Muhtasari
  • Mwilu ateuwa majaji 3 kusikiza maombi dhidi ya Kananu
  • Benchi litaongozwa na Jaji Said Chitembwe
  • Mnamo Januari mwaka huu, Jaji Antony Mrima alijumuisha kesi zote 10 za kupinga uhakiki, uteuzi, kuapishwa na kuchukua ofisi ya Ann Kananu kama Gavana wa Kaunti ya Nairobi
Afisa mkuu wa tume ya IEBC kaunti ya Nairobi Joseph Eroo alipomkabidhi cheti cha uteuzi Anne Kananu Mwenda aliyekuwa ameteuliwa kuwa naibu gavana.
Afisa mkuu wa tume ya IEBC kaunti ya Nairobi Joseph Eroo alipomkabidhi cheti cha uteuzi Anne Kananu Mwenda aliyekuwa ameteuliwa kuwa naibu gavana.
Image: GPS

Kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu ameteua Benchi la majaji watatu kusikiliza maombi yaliyowasilishwa dhidi ya Naibu Gavana wa Nairobi Ann Kananu Mwenda.

Benchi litaongozwa na Jaji Said Chitembwe.

Majaji wengine walioteuliwa kwenye benchi hilo ni Weldon Korir na Wilfrida Okwany.

 

Kesi hizo zitatajwa Februari 25 saa sita mchana kabla ya benchi lililotajwa.

Mnamo Januari mwaka huu, Jaji Antony Mrima alijumuisha kesi zote 10 za kupinga uhakiki, uteuzi, kuapishwa na kuchukua ofisi ya Ann Kananu kama Gavana wa Kaunti ya Nairobi.

Mrima aliunganisha kesi zote akisema itaokoa wakati wa kimahakama na kupeana kila chama fursa ya kusikilizwa.

"Ili kukuza mwenendo mzuri wa mambo haya yote yanayohusiana na kupewa muda mdogo wa kimahakama pamoja na hitaji la kupeana kila chama fursa ya kusikilizwa, nina msimamo kwamba mambo haya yote yaimarishwe," alisema jaji.

Miongoni mwa maombi 10, ni yale yaliyowasilishwa na Okiya Omtatah, Chama cha Wanasheria cha Kenya, Thirdway Alliance, Anne Kananu mwenyewe kati ya wengine.