KPLC mashakani baada ya twiga wawili kupigwa na umeme

Muhtasari

• Siku ya Ijumaa asubuhi, twiga walipigwa na umeme. Jumamosi, twiga mwingine alikufa mahali hapo.

Shirika la Kenya Power linatathmini hali katika hifadhi ya wanyama ya Syosambu huko Nakuru baada ya kifo cha twiga watatu.

Katika taarifa siku ya Jumatatu, KWS ilisema Kenya Power inatarajiwa kuchukua hatua kuweka nguzo refu za nyaya za stima ili kuzuia umeme kuangamiza twiga ndani ya hifadhi hiyo.

"Ripoti za awali zinaonyesha kuwa urefu wa nguzo za nyaya za umeme zinazovuka eneo hilo ni wa chini ikilinganishwa na urefu wa twiga," KWS ilisema.

Ilibaini kuwa Waziri wa Utalii Naib Balala pia anamshirikisha Waziri wa kawi Charles Keter kupata suluhisho la kudumu.

Twiga hao watatu walipigwa na umeme katika Hifadhi ya Soysambu, na kufikisha 11 idadi ya twiga ambao wameuawa kwa sababu umeme katika mbugha hiyo.

Siku ya Ijumaa asubuhi, twiga walipigwa na umeme. Jumamosi, twiga mwingine alikufa mahali hapo.

"Tunaamini ilikwenda mahali hapo baada ya kupata harufu ya damu," duru zilisema.

Duru zilisema kwamba mizoga miwili ya kwanza ilikuwa imeondolewa mbali na nyaya za umeme ili kuzuia ndege aina ya tai na twiga wengine kuja mahali hapo kuomboleza.