Mudavadi adai Raila ni mlaghai wa kisiasa

Muhtasari

• Kinara wa ANC Musalia Mudavadi alimtaja Raila kama mlaghai wa kisiasa na alidai kuwa ‘handshake’ ilipangwa mapema kabla ya kura ya urais kurudiwa mwezi Oktoba 2017.

Vinara wa NASA
Vinara wa NASA

Majibizano makali yameibuka kati ya kiongozi wa ODM Raila Odinga na wenzake nwaliokuwa katika muungano wa Nasa, na kudidimiza matumaini ya wao kumuunga mkono mgombea mmoja wa urais kukabiliana na Naibu Rais William Ruto.

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi alimtaja Raila kama mlaghai wa kisiasa na alidai kuwa ‘handshake’ ilipangwa mapema kabla ya kura ya urais kurudiwa mwezi Oktoba 2017.

Mzozo wa hivi punde ulizuka baada ya Raila kutangaza kwamba hatamuunga mkono yeyote kuwania urais mwaka 2022 na kuwaita wenzake katika NASA waoga kwa kuhepa hafla ya kuapishwa kwake kwake kama rais wa watu.

Musalia alisema matamshi ya Raila yalisheheni udanganyifu na ulaghai wa hadhi ya juu usioweza kusikika na kudai alidanganya "kuapishwa kinyume cha sheria ili kuharakisha hamu yake ya hanshake " na Rais Uhuru Kenyatta.

Kwa mara ya kwanza, Musalia alidai Raila alijiondoa katika uchaguzi wa marudio ya urais baada ya kufanya mazungumzo ya maafikiano na Uhuru.

 "Lakini kuna uwoga zaidi katika kujiondoa kwenye uchaguzi wa marudio, uliofichwa chini ya maandamano ya kupinga matokeo ya wizi, wakati kwa kweli ni kwa sababu kitendo hicho ni sehemu ya suluhu aliyopanga mwenyewe," Musalia alisema kupitia msemaji wake Kibisu Kabatesi.

Lakini ODM ikijibu, ikimtaja Musalia kama mwanasiasa aliyeshindwa ambaye Raila alimshinda katika kaunti 46 alipogombea urais peke yake mwaka 2013.

Katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna alitaja muungano huo mpya unaowaleta pamoja Musalia, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na Moses Wetang'ula kama "Raila niachie Alliance".

Alisema watatu hao lazima waache "kucheza karibu na vibanda vyao vya kijiji na kusafiri pembe zote za nchi" kutafuta urais.

“Tunawashauri watatu hao kwamba ikiwa wanataka urais, Raila hatumii kura ya nyumbani kwake. Lazima waache kucheza karibu na vibanda vyao vya kijiji na kusafiri kwa upana wa nchi wakitafuta uungwaji mkono.

Raila amejitolea kumsaidia Rais atimize ajenda ya umoja kwa Wakenya wote, na kujenga madaraja kwa mustakabali mzuri, "Sifuna alisema, na kuongeza kuwa Raila havutiwi na mazungumzo yoyote ya 2022.

Mwaka 2002, Sifuna alisema, Musalia alikimbia vugu vugu la Rainbow Alliance na kurudi kuwa Makamu wa rais miezi mitatu wakati nchi nzima ilikuwa ikirekebisha siasa zake na kutafuta mwanzo mpya.

Musalia alisema Wakenya wanapaswa kujiuliza ni nini mtu asiye na uwezo wa kuweka marafiki anaweza kutumia mamlaka ikiwa atayapata.