Washukiwa 2 wa ugaidi wakamatwa Isiolo

Muhtasari

• Washukiwa wawili wamekamatwa wakiwa na bunduki moja aina ya AK47, risasi 128 na mabomu mawili ya mkono huko Merti, Kaunti ya Isiolo.

Washukiwa wawili wamekamatwa wakiwa na bunduki moja aina ya AK47, risasi 128 na mabomu mawili ya mkono huko Merti, Kaunti ya Isiolo.

Abdi Fatah Ibrahim na Yusuf Mohamed walikamatwa baada ya polisi waliokuwa wakishika doria katika eneo hilo kuona magari mawili waliyoyashuku aina ya Toyota Probox.

Kikosi cha pamoja cha maafisa kutoka DCI Merti na Yamicha Police Post kiliwaagiza washukiwa kusimama, lakini badala yake magari hayo mawili yakaenda kwa kasi.

Polisi hao waliyafuata magari hayo na ndiposa  watu wawili katika moja ya magari hayo lenye nambari za usajili KCY 576H kuanza kuwaifyatulia risasi maafisa hao.  Maafisa hao walijibu kwa kufyatulia risasi gari la washukiwa.

washukiwa walijisalimisha na kukamatwa. Waliposaka gari hilo jwalipatasilaha hizo, sare za kijeshi, simu mbili za rununu na visu kadhaa.

DCI George Kinoti alisema gari lingine lilifanikiwa kutoroka, lakini wapelelezi wanalisaka.

Washukiwa waliokamatwa wanaendelea kuhojiwa, huku Kitengo cha mabomu na Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi kikifuatilia kesi hiyo.